Kwa
tafsiri daraja (kwa kiingereza “bridge”)
inaunganisha pande mbili ambazo zilikuwa na
kikwazo. Kwa tafsiri rahisi ya maajabu, daraja inaondoa vikwazo vya
mawasiliano na kuleta uelewano katika pande mbili ambazo awali
zilitengana.
Daraja ni kielelzo cha
utu, inaleta umoja,
uwazi na kuasaidiana. Daraja inaleta mwingiliano
wa mawazo, bidhaa na
mambo mbalimbali yanayochochea mabadiliko
katika mtu mmoja mmoja na hatimae
jamii nzima. Hivi ndivyo shule ya awali ya Bridge Preschool
ilivyodhamiria kulea watoto katika kijiji kidogo cha Lugalo na
kuwaunganisha na ulimwengu mzima katika tamaduni mbalimbali ambazo
zitaleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii ya watanzania
na ulimwengu mzima.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni