Kuhusu sisi


Bridge preschool ni shule ya awali ya English Medium. Shule hii ipo katika kijiji cha lugalo, kusini mashariki mwa Tanzania. Ni shule pekee inayojikita katika kuwajengea uwezo watoto uwezo wa kielimu Shule inatoa mazingira rafiki ya kielimu, kijamii na uwezo wa kupambanua mambo mbalimbali. Tunaamini umri wa awali wa mtoto ni umri mathubutu katika maendeleo ya mtoto kitaaluma na stadi za kijamii. Lengo letu ni kuwapatia wigo mpana watoto kujua fursa, kupanua mawazo na malengo ili wawezo kuiona dunia na jamii katika upana wake. Tunawalea watoto kupata maarifa ya tofauti ya tamaduni mbalimbali za jamii katika sayari hii ili waweze kukua na ufahamu wa kujitambua na kuheshimu jamii nyingine duniani.

Kwa kufahamu mazoea na tamaduni mbalimbali, watoto wetu watapata ubunifu wa kutumia tofauti zetu kujenga upendo na malengo ya pamoja kwa uhuru zaidi katika historia yeyote ile ya mwanadamu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni